• TAMICO

    Wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Arusha/Manyara/Kilimanjaro/Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na kaimu katibu Mkuu Mama Masaida Chiwinga(Suti Nyeusi) aliyeketi kati kati nawa pili kutoka kushoto ni mwenyekiti wa wanawake kanda ya kaskazini watatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa kanda ya kaskazini.

  • TAMICO

    Watendaji wakuu wa taifa (KUT)

...1 ...1

TAMICO

Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na Kazi Nyinginezo; kwa kifupi TAMICO ni chama cha cha wafanyakazi kilichoundwa na wafanyakazi wenyewe kwa lengo la kutetea, kulinda na kuboresha haki na maslahi ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika sekta za Migodini, Nishati, Ujenzi na kazi nyinginezo zinazotoa huduma saidizi katika sekta za Migodi, Nishati na Ujenzi. Kwa maana nyingine TAMICO ni mali ya wanachama wenyewe.

Dira Ya Chama

Kila mfanyakazi anastahili haki ya kazi yake, heshima na kuthaminiwa kwa utu wake na kwamba wafanyakaziwote duniani ni sawa.

Malengo ya chama

Kuwaunganisha, kuwaelimisha, kulinda na kutetea haki na maslahi ya Wafanyakazi wote walioajiriwa katika sekta ya za migodi, Nishati, Ujenzi na kazi nyinginezo kwa madhumunui ya kuimarisha uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.

IMANI YA CHAMA

  1. Wafanyakazi wote duniani ni sawa.
  2. Kila mfanyakazi anastahili haki ya kazi yake, heshima na kuthaminiwa kwa utu wake
  3. Mshikamano wa dhati wa wafanyakazi popote pale ndiyo ngao pekee ya kuleta, kulinda na kudumisha umoja wao
  4. Utengano wa aina yoyote kati ya wafanyakazi ni kielelezo cha udhauifu.
  5. Umoja utatuwezesha kujadiliana na mwajiri kwa kujiamini kwa uhakika. Utengano utasababisha unyonge , kuonewa kunyanyaswa na kudhulumiwa.