MAJUKUMU YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI

  1. Kuwaingiza,kuwalinda na kuwaunganisha ndani ya chama kimoja ch wafanyakazi wote walioajiriwa katika sekta za migodi, nishati, ujenzi na kazi nyinginezo kwa madhumuni ya kuimarisha uchumi na ustawi wao kudai kutetea na kulida haki na maslahi yao.
  2. Kujadiliana na waajiri na kufikia muafaka juu ya kuborehsa ajira na hali bora sehemuza kazi kwa kuingia mikataba au kwa kutumia njia nyingine za kisheria.
  3. Kulinda usalama wa ajira ya wanachama kwa njia ya kusuluhisha kwa kutatua malalamiko au migogoro ya kikazi kati ya waajiri na wanachama.
  4. Kukuza umoja na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi katika sekta za migodi, nishati, ujenzi na kazi nyinginezo.
  5. Kuhakikisha kwamba wanachama na waajiri wanasimamia vyema miktaba ya ajira iliyofungwa baina yao, utekelezaji wa sheria na kanuni, utatuzi wa migogoro, taratibu za kazi, kufungwa na kutekelezwa kwa mikataba ya kutambuana na mikataba ya hali bora za kazi na kuundwa kwa mabaraza ya kazi.
  6. Kuwaelimisha wanachama juu ya chama chao, haki na wajibu wao, sheria za kazi na kuwapa ushauri wa kisheria wanapohitaji.
  7. Kuwa na mawasiliano na uhusiano mwema na vyama vingine vya wafanyakazi, mashirikisho ya vyama vya wafanyakazi na mashirika mengine ya mwafanyakazi yaliyopo nje ya nchi,kwa faida ya wanachama na chama.
  8. Kushauriana na umoja wa waajiri ulioundwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni zake kwa madhumuni ya kudumisha uhusiano mwema kati ya waajiriwa na wanachama.
  9. Kushughulika mambo mengine yote ambayo hayapingani na katiba hii na sheria za nchi.