Jinsi ya Kujiunga na Tamico

Uanachama

Wanachama watakuwa ni wafanyakazi katika Sekta za Migodi, Nishati, Ujenzi na Kazi Nyinginezo ambao kwa hiari yao wamejiunga na Chama. Mfanyakazi aliyeamua kwa hiari yake kujiunga na Chama kwa mujibu wa Katiba hii, kanuni za chama, sheria ya kazi na kanuni zake.

Kiingilio

Baada ya kukubali kujiunga katika chama mwanachama atalipa kiingilio katika kiwango kitakachowekwa na Baraza kuu.Mwanachama atakapolipa kiingilio atapewa kadi ya uanachama.Kiingilio kikishalipwa hakitarudishwa kwa sababu yoyote ile.

Ada

Mwanachama ataanza kulipa Ada ya kila mwezi katika kiwango kitakachowekwa na Baraza kuu kwa mujibu wa katiba na kwa kuzingatia sheria ya kazi.